HomeRadio Vaticana
foto testata  

Categories


  Charity & Solidarity


  Church


  Culture & Society


  Vatican Documents


  Synod


  Ecumenism


  Family


  Youth


  Justice & Peace


  Politics


  Religion & Dialogue


  Science & Ethics


  Audiences
   & Angelus



  Pastoral visits


cx_t06

CTV - You tube

CTV

 home > Church > news


21/12/2010 8.14.11



Dr. Ralamboarison, mwanamke wa kwanza kuwa Katibu mkuu wa Shirika la Kipapa la Utoto Mtakatifu






Kardinali Ivan Dias, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa watu amemteua Dr. Baptistine Jeanne Ralamboarison, mwanachama wa Chama cha kitume cha Papa Sylvester, kuwa Katibu mkuu mpya wa Chama cha Kitume cha Kipapa kwa ajili ya Utoto Mtakatifu. Dr. Ralamboarison anakuwa ni mwanamke wa kwanza kushika wadhifa wa juu kabisa katika Chama cha Kitume cha Kipapa kwa ajili ya Utoto Mtakatifu. Alizaliwa tarehe 6 Mei, 1951, huko Madagascar. Baada ya masomo yake ya msingi na sekondari, alifanikiwa kujiendeleza zaidi nchini Ufaransa na kujipatia shahada katika masomo ya lugha na sheria.

Alianza kutekeleza utume wake kwenye Baraza la Kipapa la Utoto Mtakatifu kunako mwaka 1983, wakati huo Sekretarieti ya Chama hiki ilipohamishwa kutoka Paris, Ufaransa na kuwekwa Makao Makuu ya Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa watu, lililoko mjini Roma. Uteuzi huu unaodumu kwa kipindi cha miaka mitano, umeanza rasmi hapo tarehe 1 Desemba, 2010.

Baraza la Kipapa la Utoto Mtakatifu, lilianzishwa tarehe 19 Mei, 1843 na Askofu Charles August Marie De Forbin-Janson wa Jimbo la Nancy, Ufaransa, kwa lengo la kutoa elimu itakayowawezesha watoto kujenga ndani mwao moyo na ari ya kimissionari; kwa kutambua na kujitahidi kujinyima kwa ajili ya kusaidia mahitaji ya watoto wengine wanaoishi katika shida na mahangaiko mbali mbali kwenye nchi za Kimissionari duniani. Chama hiki cha kitume, kilianza kuenea kwa haraka, kutokana na kuungwa mkono na Mashirika mbali mbali ya liyokuwa yanatoa elimu kwa watoto.

Baba Mtakatifu Leo wa kumi na tatu, katika barua yake ya kichungaji ya mwaka 1880 aliwapongeza waanzilishi hawa kwa kujitahidi kuwaandaa watoto katika utakatifu wa maisha kadiri ya mapenzi ya Mungu. Baba Mtakatifu Pio wa kumi na moja, akakitangaza Chama hiki cha Kitume kuwa na hadhi ya kipapa, hapo tarehe 3 Mei, 1922. Kila mwaka wakati wa maadhimisho ya Siku kuu ya Tokeo la Bwana, Wanachama wa Utoto Mtakatifu, husali kwa pamoja na kujitahidi kukusanya fedha kwa ajili ya mahitaji ya watoto wenzao sehemu mbali mbali za dunia, wakiongozwa na kauli mbiu "watoto kuwasaidia watoto wenzao".

Fedha inayokusanywa kila mwaka, kutokana na majitoleo ya watoto hao na mchango kutoka kwa watu wenye mapenzi mema, imekuwa ni kichocheo kikuu cha maendeleo ya watoto katika sekta ya elimu, afya, chakula na malazi, pamoja na kusimama kidete kulinda na kutunza zawadi ya maisha kwa watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi.

Hata katika nchi nyingi za Kiafrika, Shirika la Utoto Mtakatifu linaanza kushika kasi, kwani Maaskofu wengi wanatambua na kuheshimu mchango wa watoto katika sala na majiundo yao kwa siku za usoni. Waswahili husema, "mtoto umleavyo ndivyo akuavyo."


  « back to index

 




















Related categories


Page précédente  Previous page
Page d'accueil  Home Page
Ecrire à la rédaction  Contact us
top
top
All the contents on this site are copyrighted ©. Webmaster / Credits / Legal Conditions
top
top