HomeRadio Vaticana
foto testata  

Categories


  Charity & Solidarity


  Church


  Culture & Society


  Vatican Documents


  Synod


  Ecumenism


  Family


  Youth


  Justice & Peace


  Politics


  Religion & Dialogue


  Science & Ethics


  Audiences
   & Angelus



  Pastoral visits


cx_t12

CTV - You tube

CTV

 home > Justice & Peace > news


15/12/2010 8.49.44



Jitahidini kuheshimu na kuthamini utu wa mwanadamu, kiungo makini cha upendo na mshikamano ndani ya jamii






Mheshimiwa Padre Vincent Mhina, mtaalam wa masuala ya utu na heshima ya mwanadamu, ambaye pia ni Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Teresia wa Mtoto Yesu, Jimbo Kuu la Arusha, katika utafiti wake anasema, Kanisa linapenda kukazia juu ya thamani na heshima ya mwanadamu kwa vile wameumbwa kwa sura na mfano wa Mungu na kukombolewa na Yesu Kristo kwa njia ya mateso, kifo na ufufuko wake.

Utu na heshima ya mwanadamu haijalishi dini yake, kwani waswahili husema "mtu ni utu na wala si dini yake". Wakristo kwa namna ya pekee, wanauangalia utu na heshima ya mwanadamu ulioinuliwa na kupewa hadhi ya juu kabisa kwa njia ya Fumbo la Umwilisho, Neno wa Mungu, alipoutwaa mwili na kukaa kwake Yeye Bikira Maria, akawa mwanadamu, katika mambo yote isipokuwa hakutenda dhambi. Tukio hili likamwezesha Bikira Maria kuwa ni Tabernakulo ya kwanza ya Neno wa Mungu aliyefanyika mwili.

Yesu Kristo mwenyewe katika maisha yake ya hadhara, alipokuwa anatangaza Habari Njema ya Wokovu kwa njia ya ushuhuda wa maisha yake, aliwaonesha upendo na huruma wote waliokuwa wananyanyasika na kutengwa ndani ya jamii; wagonjwa na wahitaji wakaonja uwepo wake na wenye dhambi wakaponywa majeraha yao ya dhambi. Kila mtu aliheshimiwa na kuthaminiwa utu wake, Yesu akawa ni kielelezo hai cha: upendo, huruma, msamaha na mshikamano kati ya watu na hivyo kuvunja kuta zote za utengano zilizojengeka kutokana na hisia na matabaka ya watu.

Padre Mhina anasema, maadili ya utu na heshima ya mtu, yanawachangamotisha watu kuona na kuthamini utu wa mtu, kinyume kabisa na mwelekeo wa sasa unaowaonesha watu kupenda mno vitu na kusahau utu, kiasi cha kuwafanya waswahili kusema, "hapa hapendwi mtu, isipokuwa pochi yake". Kwa kuheshimu na kuthamini utu wa mwanadamu; heshima hii pia anapewa Yeye aliyeasili ya kazi kuu ya uumbaji ambaye ni Mwenyezi Mungu. Huwezi kumnyanyasa na kumdhulumu jirani yako wakati huo huo ukijidai kwamba, unampenda Mwenyezi Mungu. Upendo kwa jirani ni kielelezo cha kweli kwa upendo wa Mungu.


  « back to index

 




















Related categories


Page précédente  Previous page
Page d'accueil  Home Page
Ecrire à la rédaction  Contact us
top
top
All the contents on this site are copyrighted ©. Webmaster / Credits / Legal Conditions
top
top