HomeRadio Vaticana
foto testata  

Categories


  Charity & Solidarity


  Church


  Culture & Society


  Vatican Documents


  Synod


  Ecumenism


  Family


  Youth


  Justice & Peace


  Politics


  Religion & Dialogue


  Science & Ethics


  Audiences
   & Angelus



  Pastoral visits


cx_t15

CTV - You tube

CTV

 home > Science & Ethics  > news


18/11/2010 11.30.25



Mkutano wa XXV Kimataifa: Utume wa kinabii katika masuala ya afya, dhamana ya Serikali, mshikamano na tatizo la haki miliki






Kardinali Tarcisio Bertone, Katibu mkuu wa Vatican, akizungumza kwenye mkutano wa ishirini na tano wa kimataifa, ulioandaliwa na Baraza la Kipapa la wahudmu wa sekta ya afya anakazia kimsingi mambo makuu manne, yanayobainishwa kwenye hati ya kichungaji ya Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, upendo katika ukweli: utume wa kinabii wa Mama Kanisa; dhamana ya Serikali, Umuhimu wa mshikamano unaoongozwa na kanuni auni; tatizo la haki na haki miliki ya kiakili.

Mama Kanisa katika utume wake wa kinabii, anayo dhamana ambayo anaendelea kuifanyia kazi kwa kuhakikisha kwamba, utu na heshima ya mwanadamu vinalindwa na kuthaminiwa na kwamba, mwanadamu anapaswa kuwa ni kiini cha maendeleo yanayozingatia kanuni msingi za kimaadili; mafao ya wengi, utu na heshima yake. Kanisa ni Familia ya Mungu inayowajibika na inapania kuona kwamba, misingi hii inatekelezwa katika maisha na utume wake.

Serikali zinawajibu wa kutoa huduma bora ya afya kwa wananchi wake mintarafu sheria na kanuni zilizoainishwa na Jumuiya ya Kimataifa, kwa kutambua kwamba, afya bora ni sehemu ya haki msingi za binadamu na inapaswa kutekelezwa kwa kushirikiana na sekta mbali mbali za maisha ya mwanadamu, ili aweze kufikia ukomavu mkamilifu. Hii ni changamoto ya kulinda na kutetea zawadi ya maisha ya mwanadamu aliyeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu.

Kardinali Bertone anasema, myumbo wa uchumi wa kimataifa na mikakati ya uchumi isiwapokonye wananchi haki yao msingi ya kupata huduma bora ya afya, kwani wagonjwa ni kati ya watu wanaopaswa kuonjeshwa upendo na haki. Serikali zinawajibu kisheria, kiutawala na kiuchumi, kuhakikisha kuwa haki hizi zinatekelezeka kwa watu wake.

Rasilimali, matokeo ya tafiti na wataalam wa sekta ya afya waliopo wanapaswa kutumiwa vyema kwa ajili ya kulinda na kutetea mafao ya wengi badala ya ubadhirifu na matumizi mabaya ya rasilimali hii. Nchi zilizoendelea zina wajibu pia wa kujenga utamaduni wa mshikamano ili watu wengi waweze kupata huduma bora ya afya, kwani kwa pamoja na wanaunda Familia ya Mungu. Mshikamano huu unafumbatwa katika kanuni ya auni.

Msaada wa kiuchumi unaotolewa kwa nchi maskini usiwe na masharti magumu na masilahi kwa nchi wahisani, bali wadau wote washirikishwe kuanzia ngazi ya chini kabisa. Kardinali Bertone anasema, kuna vikwazo vikubwa ambavyo vinawekwa kutokana na hati miliki ya watengenezaji wa dawa na taaluma zao hasa katika sekta ya afya. Mwelekeo huu umekuwa ni wa kutafuta faida zaidi na wala si kwa ajili ya mafao ya wengi, hali inayochangia ongezeko la baa la umaskini duniani. Mshikamano wa dhati unaweza kupunguza vikwazo hivi na hivyo huduma ya afya ikaboreka zaidi.


  « back to index

 




















Related categories


Page précédente  Previous page
Page d'accueil  Home Page
Ecrire à la rédaction  Contact us
top
top
All the contents on this site are copyrighted ©. Webmaster / Credits / Legal Conditions
top
top