HomeRadio Vaticana
foto testata  

Categories


  Charity & Solidarity


  Church


  Culture & Society


  Vatican Documents


  Synod


  Ecumenism


  Family


  Youth


  Justice & Peace


  Politics


  Religion & Dialogue


  Science & Ethics


  Audiences
   & Angelus



  Pastoral visits


cx_t10

CTV - You tube

CTV

 home > Family > news


04/11/2010 9.17.36



Familia ni kitovu cha amani na upendo






Askofu mkuu Josè De Queioros Alves wa Jimbo kuu la Huambo, Angola, hivi karibuni, amezitaka familia kujenga mazingira yatakayoziwezesha kuendelea kuwa ni wadau wakuu katika kazi ya uumbaji waliyokabidhiwa na Mwenyezi Mungu, kwa kujenga na kudumisha mazingira ya amani na upendo wa dhati.

Askofu De Queiròs Alves ameyasema hayo wakati alipokuwa anazungumza na washiriki wa mkutano wa nne ngazi ya kijimbo, uliokuwa unajadili kuhusu umuhimu wa kudumisha tunu msingi za maisha ya kifamilia. Amewataka wajumbe kufanya tafakari ya kina kuhusu hali halisi ya familia katika ulimwengu mamboleo, ili hatimaye, kujenga mazingira yatakayoharakisha amani, upendo na mshikamano wa dhati, kila mtu akijitahidi kutekeleza wajibu wake, ili kuboresha maisha ya kifamilia.

Hii ndiyo changamoto kubwa inayoendelea kuzikabili familia za kikristo katika ulimwengu mamboleo, ili hatimaye, ziweze kusimama kidete: kulinda na kutetea tunu msingi za kifamilia kwa ajili ya mafao ya Jamii nzima. Ni mwaliko wa kusaidiana ndani ya familia, ili kujenga upendo wa kweli na fadhila nyingine za kikristo. Familia kwa hakika anasema Askofu De Queiròs inapaswa kusimama kidete kulinda zawadi ya maisha dhidi ya utamaduni wa kifo, kwa kutekeleza majukumu yake na hatimaye, kutafuta suluhu ya matatizo wanayokumbana nayo katika mwanga wa Kiinjili.


  « back to index

 




















Related categories


Page précédente  Previous page
Page d'accueil  Home Page
Ecrire à la rédaction  Contact us
top
top
All the contents on this site are copyrighted ©. Webmaster / Credits / Legal Conditions
top
top