27/10/2010 11.31.06


Wahukumiwa adhabu ya kifo nchini Kenya kwa mauaji ya Padre Bertaina


Mheshimiwa Padre Franco Cellana, Mkuu wa Shirika la Waconsolata Kanda ya Afrika Mashariki, aliyekuwa anafuatilia kwa makini kesi ya mauaji ya Padre Giuseppe Bertaina yaliyotokea tarehe 16 Januari, 2009, Jijini Nairobi, Kenya, anasema, wao wamewasamehe watuhumiwa dhambi zao, lakini sheria inapaswa kuchukua mkondo wake baada ya ufanisi mkubwa katika uchunguzi na hatimaye, watuhumiwa kutiwa mbaroni.
Felix Savayi Kwesha na Mabel Kavati, tarehe 22 Oktoba, 2010, Mahakama iliwatia hatiani na hivyo kuhukumiwa adhabu ya kunyongwa hadi kufa. Kanisa Katoliki katika mafundisho yake Jamii, linapinga adhabu ya kifo, kwani inakwenda kinyume na haki msingi za binadamu.
|