HomeRadio Vaticana
foto testata  

Categories


  Charity & Solidarity


  Church


  Culture & Society


  Vatican Documents


  Synod


  Ecumenism


  Family


  Youth


  Justice & Peace


  Politics


  Religion & Dialogue


  Science & Ethics


  Audiences
   & Angelus



  Pastoral visits


cx_t13

CTV - You tube

CTV

 home > Politics  > news


12/10/2010 8.54.57



Mbinu mkakati wa kupambana na baa la njaa, utapiamlo na umaskini duniani!






Jumuiya ya Kimataifa kwa muda wa juma zima, kuanzia Jumatatu tarehe 11 hadi 15 Oktoba, 2010 inakutana ili kujadili pamoja na mambo mengine: hali ya usalama wa chakula duniani; athari za kuchechemea kwa uchumi wa kimataifa, changamoto kutoka kwa makampuni ya kigeni yanayowapokonya wananchi maeneo makubwa ya ardhi hasa katika nchi maskini zaidi duniani.

Mashirika makuu ya Umoja wa Mataifa yanayojihusisha na masuala ya chakula na kilimo yanachambua kwa kina hali ya usalama wa chakula duniani, mkutano ambao unatarajiwa kuhitimishwa hapo tarehe 15 Oktoba, katika mkesha wa kilele cha maadhimisho ya Siku ya chakula duniani hapo tarehe 16 Oktoba, 2010.

Kwa mara ya kwanza mkutano huu unahudhuriwa na wajumbe kutoka katika vyama vya kiraia na mashirika yasiyo ya kiserikali, kama sehemu ya mabadiliko makubwa yaliyofanywa kwenye kamati ya kimataifa inayoshughulikia hali ya usalama wa chakula duniani. Lengo ni kuibuka na mbinu mkakati utakaosaidia kupambana na baa la njaa duniani, kwa kuboresha sera za kilimo, ugavi wa misaada ya maendeleo pamoja na kudumisha uhusiano mwema baina ya nchi wanachama.

Mkutano huu unafanyika wakati ambapo bei ya mazao ya nafaka inaendelea kuongezeka maradufu, kama ile iliyojitokeza mwezi Juni, 2008 wakati wa kilele cha kuchechemea kwa uchumi wa kimataifa. Akiwakaribisha wajumbe katika mkutano huu, Dr. Jacque Diouf, mkurugenzi mkuu wa FAO amewakumbusha wajumbe kwamba, changamoto ya usalama wa chakula duniani inahitaji mbinu mkakati wa kimataifa na maeneo husika, ili kupata majibu ya pamoja.

FAO inapenda kuhakikisha kwamba, baa la njaa linatokomezwa duniani kwa kutumia wataalam wake wanaopaswa kushirikiana na wadau wengine katika sekta ya kilimo. Dr. Diouf anasema kwamba, umefika wakati kwa Jumuiya ya Kimataifa kupambana kufa na kupona na baa la njaa, utapiamlo pamoja na umaskini. Hadi sasa kuna jumla ya nchi thelathini ambazo zinakabiliwa na uhaba wa chakula na kwamba, wanahitaji chakula cha msaada. Jumuiya ya Kimataifa inapaswa kujifunga kibwebwe ili kudhibiti kuporomoka kwa tija na uzalishaji katika sekta ya kilimo.


  « back to index

 




















Related categories


Page précédente  Previous page
Page d'accueil  Home Page
Ecrire à la rédaction  Contact us
top
top
All the contents on this site are copyrighted ©. Webmaster / Credits / Legal Conditions
top
top