HomeRadio Vaticana
foto testata  

Categories


  Charity & Solidarity


  Church


  Culture & Society


  Vatican Documents


  Synod


  Ecumenism


  Family


  Youth


  Justice & Peace


  Politics


  Religion & Dialogue


  Science & Ethics


  Audiences
   & Angelus



  Pastoral visits


cx_t06

CTV - You tube

CTV

 home > Church > news


24/09/2010 14.31.05



Wakristu Sudan watumainia Kura ya maoni






Alhamis hii, Sudan ilisubiri kwa hamu kutoa mchango wake kwa hamu , ndani ya Umoja wa Mataifa ambamo Umoja unazungumzia haki ya Wasudan, kupiga kura ya maoni, kama hatua muhimu itakayotoa maamuzi ya wengi, katika hoja ya eneo la Kusini mwa Sudan, kujitenga na Kaskazini.

Upigaji a kura hiyo muhimu ya maoni, unaotazamiwa kutekelezwa January 2011, ikiwa imepita miaka kumi, tangu kusitishwa kwa vita kati ya wapiganaji wa eneo la Kusini ambao wengi wao ni Wakristu na watu wa imani za kijadi na wakazi wa eneo la Kaskazini ambao wengi wao ni Waislamu na waarabu. Makubalianao ya kusirtisha vita kati ya pande hizi yalitwa sahihi mwaka 2005.

Habazi zinabainisha kwamba, Jumuiya ya kimataifa bado ina wasiwasi na matokeo ya kura ya maoni itakayopigwa , kutokana na wasiwasi kwamba, inaweza kuzua vita vingine kama matokeo yatakuwa kinyume na matazamio ya wengi.

Askofu Cesare Mozzalari , wa jimbo la Rumbek , Kusini mwa Sudan, katika mahojiano ameutaja upigaji wa kura hiyo, kuwa ni hatua muhimu, katika kusitisha kipindi cha maonevu na unyanyasaji uliofanyika katika kipindi chamiaka ya vita.

Askofu Mozzalari , ameendelea kutaja tumaini la Kanisa katika kura hiyo kwamba, ni njia pekee ya kutenganisha tamaduni hizi mbili , ambazo daima zimekuwa zikipingana kwa kipindi kirefu na kusababisha lta maafa makubwa kwa jamii ya Wasudan hasa watu wa eneo la Kusini.

Ameitaja kampeini ya Kanisa kwa wakati huu, kwamba ni kuhimiza watu kuishi kwa amani na utulivu, kama hatua inayowahakikishia kuuitumia vyema , haki yao katika kutoa maamuzi kidemokrasia , kupitia upigaji wa kura ya maoni . Kwa utambuzi wao, watu wengi wa Kusini mw Sudan wanapenda kuona eneo la Kusini linakuwa taifa huru, kutoka eneo la Kaskazini.


  « back to index

 




















Related categories


Page précédente  Previous page
Page d'accueil  Home Page
Ecrire à la rédaction  Contact us
top
top
All the contents on this site are copyrighted ©. Webmaster / Credits / Legal Conditions
top
top