30/08/2010 10.33.28


Kanisa litaendelea kuchangia mchakato wa kuleta upatanisho, haki na amani nchini Tanzania


Vyama mbali mbali vya kisiasa nchini Tanzania, walau kwa kiasi kikubwa vimekamilisha mchakato wa kuwapata wagombea uongozi watakaosimama katika kinyang'anyiro cha uchaguzi mkuu, hapo Oktoba, 31, 2010. Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu, linasema, litaendelea kutoa mchango wake ili kuleta upatanisho, haki na amani.
Sasa tunajiunga na Padre Agapito Mhando akiwa ndani ya viunga vya Radio Vatican, kukuletea ujumbe wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, kuelekea uchaguzi mkuu, hapo tarehe 31 Oktoba, 2010.
|