HomeRadio Vaticana
foto testata  

Categories


  Charity & Solidarity


  Church


  Culture & Society


  Vatican Documents


  Synod


  Ecumenism


  Family


  Youth


  Justice & Peace


  Politics


  Religion & Dialogue


  Science & Ethics


  Audiences
   & Angelus



  Pastoral visits


cx_t12

CTV - You tube

CTV

 home > Justice & Peace > news


23/07/2010 9.13.26



Maoni ya Maaskofu Katoliki kuhusu Muswada wa Katiba Mpya ya Zambia






Baraza la Maaskofu Katoliki Zambia, limewaandikia waamini na watu wote wenye mapenzi mema nchini humo kuelezea sababu msingi zilizolifanya Baraza la Maaskofu Katoliki Zambia kujitoa katika kamati ya kitaifa ya utarashijaji wa muswada wa katiba mpya ya Zambia, changamoto zinazoukabili muswada huu, msimamo wa Maaskofu wa Zambia na maoni yao kwa siku za usoni.

Baraza la Maaskofu Katoliki Zambia linasema, muswada wa Katiba Mpya ya Zambia umekamilika, sasa wananchi wanaalikwa kutoa maoni yao. Maaskofu hawakukubali mwaliko wa Serikali kujiunga na Tume ya kuandaa muswada wa Katiba Mpya ya Zambia, kutokana na Serikali yenyewe kushindwa kuyapatia ufumbuzi masuala nyeti juu ya muswada huo.

Idadi kubwa ya wajumbe walikuwa ni wanasiasa na wawakilishi wa Serikali, ambao kimsingi, hawakufurahishwa na mapendekezo yaliyokuwa yametolewa na Kamati ya Mung'omba. wajumbe hao walionesha mwelekeo hasi kuhusu sheria ya haki msingi za kiuchumi na kijamii, uchaguzi wa Rais, uteuzi wa mawaziri kutoka nje ya Bunge pamoja na kumpunguzia Rais madaraka.

Maaskofu wanaonesha wasi wasi wao kwamba, kutokana na mapungufu yanayojitokeza kwenye muswada huu, Je, wajumbe hao watalazimika kuandaa upya muswada huu; kwa vile baadhi ya wajumbe wa kamati hii walikuwa pia ni wabunge, Je, Bunge litaweza kuupitisha muswada huu kuwa sheria? Je, wananchi wa Zambia watashirikishwa katika maamuzi yao kama wanakubaliana au kuukataa muswada wa Katiba Mpya ya Zambia kwa njia ya Kura ya Maoni? Haya ni baadhi ya maswali ya msingi wanayojiuliza Maaskofu Katoliki nchini Zambia.

Maoni na mapendekezo yaliyokuwa yametolewa na wananchi hayakuzingatiwa kwenye muswada mpya wa Katiba ya Zambia. Hii inaonesha kwamba, Chama tawala, kinapenda kulinda na kudumisha masilahi yake, kinyume kabisa na matakwa ya wananchi walio wengi toka Zambia. Masuala ya haki msingi katika muswada huu hayakuguswa kabisa kama vile: malazi, chakula na huduma za afya. Uhuru wa vyombo vya habari nao uko mashakani, kwani wananchi walipendekeza kuwepo na Tume huru itakayosimamia na kudhibiti mwenendo mzima wa vyombo vya habari.

Licha ya mapungufu makubwa yanayojitokeza kwenye Muswada wa Katiba Mpya ya Zambia, lakini wanapongeza haki msingi za watu wenye ulemavu, watoto ambao bado hawajazaliwa pamoja na kupinga nyanyaso na mateso dhidi ya misingi na utu wema.

Maaskofu wa Zambia wanabainisha changamoto zinazojitokeza katika Muswada huu, ikiwa ni pamoja na ukweli kwamba, Muswada ni mkubwa mno, kinyume cha matarajio ya wengi kwamba, Katiba inapaswa kuwa ni mwongozo unaotoa kanuni msingi. Muswada wa Katiba ya sasa una maneno mengi yanayowachanganya wananchi wa kawaida. Siku arobaini zilizotengwa kwa ajili ya wananchi kuusoma Muswada ni kipindi kifupi mno kwa Katiba ambayo inapaswa kuwa ni mhimili wa maisha ya wananchi wa Zambia.

Maoni ya wananchi wa Zambia yalitolewa kwenye Tume ya Mung'omba, lakini hayakuzingatiwa! Muswada hauna uwazi, unapaswa kupigiwa kwanza kura ya maoni kabla ya kupitishwa na Bunge, ili kuepukana na makosa yaliyojitokeza siku za nyuma. Muswada haukufafanua kwa kina kipindi cha mpito baada ya uchaguzi wa Rais; ongezeko la ukubwa wa Bunge usiozingatia gharama na hali halisi ya uchumi wa nchi; uundwaji wa tume nyingi ambazo zinaegemea uteuzi wa Rais.

Baraza la Maaskofu Katoliki Zambia linasema, bado lina matumaini kwamba, Tume ya Taifa ya Kurekebisha Katiba ya Zambia itazingatia kwanza kabisa mafao ya wengi, badala ya kuendekeza masilahi ya watu wachache ndani ya nchi. Kimsingi, Muswada wa Katiba Mpya ya Zambia haukidhi matarajio ya wananchi wa Zambia, ni Muswada ambao ukipitishwa na kuwa Katiba; itapitwa na wakati mara moja.

Maaskofu wanasema, Tume hii imetumia kiasi kikubwa cha fedha na itafutika machaoni pa wananchi wa Zambia kama zilivyokuwa tume zilizotangulia bila kuzaa matunda yanayokusudiwa. Jambo hili haliwezi kuacha liendelee hivi hivi, kwani kwa sasa linagusa masuala ya kimaadili. Maaskofu wanapendekeza kwa Serikali kuunda Tume ya watalaam wachache ili kuangalia kwa makini mapungufu yanayojitokeza katika muswada wa sasa ili kuyapatia ufumbuzi wa kudumu.

Wazo hili ni la busara kuliko kuanza upya mchakato wa kuandika Muswada wa Katiba Mpya ya Zambia. Baraza la Maaskofu Katoliki Zambia linawataka wananchi kutokata tamaa, bali waendelee kuwa na matumaini kwa Katiba Mpya, itakayokidhi mahitaji ya wananchi wengi wa Zambia.


  « back to index

 




















Related categories


Page précédente  Previous page
Page d'accueil  Home Page
Ecrire à la rédaction  Contact us
top
top
All the contents on this site are copyrighted ©. Webmaster / Credits / Legal Conditions
top
top