21/07/2010 11.22.22


Mh. Padre Martin Mtambuka ateuliwa kuwa Askofu mpya wa Jimbo Jipya la Karonga, Malawi


Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, tarehe 21 Julai, 2010, ameunda Jimbo jipya la Karonga, Malawi na kumteua Mheshimiwa Padre Martin Anwel Mtumbuka kutoka Jimbo Katoliki la Mzuzu kuwa Askofu wake wa kwanza. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mteule Mtumbuka alikuwa ni Makamu wa Chuo Kikuu cha Kikatoliki Malawi.
Jimbo Jipya la Karonga limemegwa kutoka katika Jimbo la Mzuzu na litakuwa chini ya Jimbo kuu la Blantyre, Malawi. Kwa sasa lina Parokia tano, zinazohudumiwa na Mapadre wa Jimbo tisa na Mapadre watawa ni sita. Na kuna jumla ya watawa arobaini na tano. Kazi kubwa ya Uinjilishaji inatekelezwa na Makatekista ambao idadi yao kwa sasa ni thelathini na nane.
Askofu mteule Martin Anwel Mtumbuka alizaliwa tarehe 5 Augosti 1957 Kijijini Majimbula, Jimbo Katoliki la Mzuzu. Baada ya masomo yake, tarehe 31 Julai, 1988 alipewa daraja takatifu ya upadre.
|