HomeRadio Vaticana
foto testata  

Categories


  Charity & Solidarity


  Church


  Culture & Society


  Vatican Documents


  Synod


  Ecumenism


  Family


  Youth


  Justice & Peace


  Politics


  Religion & Dialogue


  Science & Ethics


  Audiences
   & Angelus



  Pastoral visits


cx_t12

CTV - You tube

CTV

 home > Justice & Peace > news


20/07/2010 9.40.01



Onesho la Picha Kampala, dhidi ya nyanyaso za kijinsia kwa wanawake na wasichana!






Umoja wa Afrika umeutenga mwaka 2010 kuwa ni Mwaka wa Amani na Usalama. Umoja huu umezindua maonesho ya picha katika kilele cha mkutano wa Umoja wa Afrika ulioanza hapo tarehe 19 na unatarajiwa kuhitimishwa hapo tarehe 27 Julai, 2010, kwa kuongozwa na kauli mbiu "Wanawake wajawazito, watoto; afya ya mtoto na maendeleo ya Afrika."

Umoja wa Afrika unapenda kuwaelimisha wananchi Barani Afrika kutambua madhara wanayokumbana nayo wanawake kutokana na migogoro ya kivita sambamba na watoto wenye umri mdogo kupelekwa kwenye uwanja wa mapambano.

Maonesho haya ya picha yanahimiza umuhimu kwa wananchi wa Afrika kuhakikisha kuwa, amani inatawala katika medani mbali mbali za maisha pamoja na kupinga vitendo vyote vya nyanyaso za kijinsia dhidi ya wanawake na watoto, vinavyotokana na ukatili wa kivita.

Umoja wa Afrika unasema kwamba, mchakato wa amani lazima uhakikishe kuwa nyanyaso dhidi ya wanawake na watoto zinasitishwa mara moja. Unaonesha pia mbinu mkakati unaoendelea kufanyiwa kazi na Umoja wa Afrika katika mapambano dhidi ya nyanyaso kwa wanawake na wasichana katika hija ya maisha yao ya kila siku.

Kwa muda wa siku mbili kuanzia tarehe 28 hadi 29 Julai, 2010, wananchi kutoka Afrika Mashariki wanapata fursa ya kutembelea na kuangalia maonesho haya, yanayoendeshwa kwa udhamini wa Idara ya amani na usalama ya Umoja wa Afrika, Shirika la Kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa, Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake wa Umoja wa Mataifa pamoja na mashirika mbali mbali ya kimataifa. Mchakato wa kukazia amani na usalama ni sehemu ya agenda nyeti za Umoja wa Mataifa.

Wakuu wa Umoja wa Afrika waliokuta mjini Tripoli, Libya kunako tarehe 31 Agosti, 2009 walitangaza kwa kauli moja kwamba, Mwaka 2010 utakuwa ni Mwaka wa Amani na Usalama Barani Afrika. Hizi ni jitihada za makusudi kabisa, zinazolenga kuwapatia wananchi fursa ya kutambua mwenendo mzima wa mchakato wa kutafuta kulinda na kudumisha amani na usalama Barani Afrika.

Umoja wa Afrika unaendelea kujivunia mafanikio yaliyopatikana kwa takribani kipindi cha miaka kumi iliyopita, lakini pia linaangalia changamoto nyingine zinazoendelea kuibuka siku hadi siku kutoka sehemu mbali mbali Barani Afrika. Lengo ni kutoa mwanya kwa wadau kuendelea kuchangia ujenzi wa harakati za amani na usalama Barani Afrika.


  « back to index

 




















Related categories


Page précédente  Previous page
Page d'accueil  Home Page
Ecrire à la rédaction  Contact us
top
top
All the contents on this site are copyrighted ©. Webmaster / Credits / Legal Conditions
top
top